1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la M23 laonekana kujiimarisha mashariki mwa DRC

6 Oktoba 2025

Waasi wa M23 wanaonekana kuimarisha utawala wao kisiasa na kiuchumi katika maeneo waliyoyateka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Goma 2025 | Viongozi wa kundi la M23 wakizungumza na waandishi wa habari
Viongozi wa M23 Corneille Nangaa, Bertrand Bisimwa, Benjamin Mponimpa na Derio Kimbulungu wakifanya mkutano na waandishi wa habari mjini Goma: 30.01.2025 Picha: Cyrile Ndegeya/Anadolu/picture alliance

Hatua hizi za M23 zinachukuliwa hasa wakati huu makubaliano ya amani yakishindwa kutekelezwa ipasavyo huko mashariki mwa  Kongo . Kundi hilo linaloungwa mkono Rwanda kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, limekuwa likiajiri maafisa na kutoza kodi, kutoa mafunzo kwa majaji, wanajeshi na polisi katika jitihada za kutengeneza utawala uliyo sambamba na uongozi wa serikali ya Kinshasa.

Eneo la mashariki mwa DRC  lenye utajiri mkubwa wa madini limekumbwa na migogoro kwa zaidi ya miongo mitatu na kusababisha maafa makubwa. Mgogoro uliongezeka baada ya kuibuka tena kwa M23 mwaka 2021 ambapo mapema mwaka huu kundi hilo lilichukua udhibiti wa miji muhimu ya Goma na Bukavu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW