Kundi la OPEC laibua hasira kwenye mkutano wa COP28
9 Desemba 2023Kundi la mataifa yanayozalisha mafuta duniani OPEC likipata dosari kuhusu msukumo kutoka kwa wafanyibiashara wa mafuta wa kuzuia uondoaji wowote katika makubaliano ya mwisho.
Soma pia: Mazungumzo ya COP28 kuamua juu ya nishati ya kisukuku?
Viongozi wa Ujerumani, Uhispania na Ufaransa wamekasirishwa na hatua ya Katibu Mkuu wa OPEC Haitham Al Ghais kutuma barua kwa wanachama 13 wa kundi hilo na washirika 10 wanaoongozwa na Urusi mapema wiki hii baada ya mazungumzo katika mkutano wa COP28 kutoa rasimu ya ahadi ambayo ni pamoja na wito wa kuondolewa kwa nishati ya visukuku.
Katika barua hiyo, Ghais alihimiza kikundi cha OPEC "kukataa maandishi yoyote ambayo yanalenga nishati ya visukuku badala ya utoaji wa gesi chafu."
Soma pia; COP28: Ahadi za kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi hazitekelezwi ipasavyo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema kuwa nchi zinazotegemea sana mafuta na gesi zinasalia kuwa kizingiti katika juhudi kubwa za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.