1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la Quad kufanya mkutano kuhusu Sudan mjini Washington

24 Oktoba 2025

Wawakilishi wa Marekani, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Misri wanakutana leo Ijumaa mjini Washington na pande husika katika vita vya Sudan, wakilenga kuzishinikiza kuelekea kwenye makubaliano ya amani.

Sudan Gedaref 2025 | Miaka 71 ya kuasisiwa kwa jeshi la Sudan
Maafisa wa jeshi la Sudan waadhimisha miaka 71 tangu kuasisiwa kwa jeshi hilo Picha: AFP

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na mazungumzo hayo chini ya mwavuli wa Quad, mkutano huo utajadili njia za kuzitaka pande zinazopigana kuheshimu usitishaji vita wa miezi mitatu uliopendekezwa kote nchini Sudan.

Kundi hilo la Quad pia linafanya juhudi za pamoja kuhakikisha misaada ya kibinadamu inafika kwa waathiriwa wa mapigano.

masuala yanayoshinikizwa na Quad 

Chanzo hicho kimeeleza kuwa wawakilishi wa mataifa hayo manne watakutana na pande hizo kwa nyakati tofauti.

Mwezi uliopita, Quad ilitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, kuruhusu misaada kuingia Sudan humo, na kuweka msingi wa usitishaji wa kudumu wa vita pamoja na mpito kuelekea utawala wa kiraia.