1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMyanmar

Kundi la waasi Myanmar ladai kukamata kamandi ya jeshi

21 Desemba 2024

Kundi la waasi wa kikabila nchini Myanmar limeyakamata makao makuu ya jeshi la nchi hiyo kwenye jimbo la Rakhine, hatua ambayo ni pigo kwa utawala wa kijeshi wa nchi hiyo.

Athari za mapigano kati ya jeshi na kundi la waasi wa AA nchini Myanmar
Athari za mapigano kati ya jeshi na kundi la waasi wa AA nchini Myanmar.Picha: AFP

Taarifa ya kundi hilo la Arakan Army (AA) imesema imechukua udhibiti kamili wa kamandi ya jeshi kwenye mji wa Ann magharibi mwa nchi hiyo jana Ijumaa, baada ya wiki kadhaa za mapigano makali. Kamandi ya Ann itakuwa ya pili kuangukia mikononi mwa waasi hao katika kipindi cha miezi mitano.

Jeshi la Myanmar linazo kamandi 14 kote nchini na nyingi kati ya hizo zinapambana hivi sasa kuyakabili makundi ya waasi ya kikabila au lile la "People's Defence Forces” lililoibuka kwa lengo la kuupinga utawala wa kijeshi ulionyakua madaraka kwa njia ya Mapinduzi mnamo mwaka 2021.

Mapigano yanalitikisa jimbo la Rakhine tangu kundi la AA lilipovishambulia vikosi vya Jeshi la Taifa Novemba mwaka jana na kuhitimisha usitishwaji mapigano ulioshuhudiwa tangu kutokea mapinduzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW