1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Kundi la Wagner ladai kuudhibiti mji wa Bakhmut

20 Mei 2023

Kiongozi wa kundi binafsi ya wapiganaji mamluki wa Kirusi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, amesema kuwa sasa, wapiganaji wake wanaudhibiti kikamilifu mji wa Bakhmut, ulio mashariki mwa Ukraine.

Kiongozi wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin na wapiganaji wake
Kiongozi wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin (mbele) akitangaza kuudhibiti mji wa Bakhmut Picha: Concord/Handout/REUTERS

Prigozhin ametoa kauli hiyo kwa njia ya video akiwa amevalia sare za kijeshi mbele ya wapiganaji walioshikilia bendera za Urusi na mabango ya kundi la Wagner.

Kwenye mkanda huo wa video video, kamanda huyo amesikika akisema kwamba wameutwaa mji wa Bakhmut majira ya saa sita mchana hii leo.

Hata hivyo, jeshi la Ukraine limekanusha tangazo la Prigozhin na limeeleza kwamba wanajeshi wake bado wanaendelea na mapambano kwenye mji huo.

Bakhmut umekuwa uwanja wa mapambano na eneo lenye umwagaji mkubwa wa damu kwa muda mrefu tangu Ukraine ilipovamiwa kijeshi na Urusi zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW