1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuondolewa vipeperushi vya wagombea kunazusha mvutano Kongo

Mitima Delachance22 Novemba 2023

Siku chache baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi, wanaharakati wa asasi za kiraia wanaonya kuhusu hali ya mvutano kati ya wafuasi wa wagombea wanaobanduwa picha na mabango ya wagombea wengine.

Wafuasi wa Mgombea urais na Rais wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo Felix Tshisekedi wakiwa na bango
Wafuasi wa Mgombea urais na Rais wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo Felix Tshisekedi wakiwa na bangoPicha: JUSTIN MAKANGARA/REUTERS

 Asasi za kiraia zinaonya kuwa ikiwa mwelekeo huo utaendelea, kuna hatari ya kuzuka ghasia na kuwataka wagombea kuwadhibiti wafuasi wao kuepusha hatari hiyo. 

Tangu mwanzo wa kampeni hiyo ya uchaguzi Novemba 19 iliopita baadhi ya wafuasi wa vyama vya mirengo yote wengi wao wakiwa ni vijana wamekuwa wakizozana mitaani haswa wakati wa kubandika picha za wagombea.

Vijana wa makundi mawili ya vyama vya kisiasa walipigana Jumapili katika maeneo ya Nguba na Muhungu walipotaka kubandika picha za wagombea wao. Kelele zilimalizika pale wapita njia walipoingilia kati kutatua mizozo yao.

Lakini baadhi ya wagombea wanasema kinachowakera zaidi ni pale picha na mabango yao yanapo banduliwa na watu wenye nia mbaya.

Soma pia:Upinzani Kongo kuafikiana juu ya kusimamisha mgombea mmoja?

Namur Mihigo Katintima ni mwanachama wa chama cha ANCE akiwa mgombeaubunge wa jimbo la Kivu kusinimjini Bukavu, anasema wanakumbwa na mshangao mkubwa wanapokutana na picha za wagombea wenzao kutoka vyama vingine ama chama zimebandikwa juu ya picha zao

"Hii ni marufuku kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi, narudia tena ni marufuku na wawajibishwe." Aliiambia Dw Kiswahili.

Asasi za kiraia Kongo zaonya sarakasi kwenye uchaguzi

Kama inavyoonekana, ni mabango ya wagombea wa vyama vya mirengo yote yanayo chanwa au kubanduliwa katika maeneo tofauti ya jimbo la Kivu kusini.

Wagombea wa nafasi ya Urais Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: AFP/Getty Images, picture alliance, G. Kusema, DW

Inaaminiwa pia kuwa hata wafuasi wa wagombea wenye itikadi moja wanachaniana picha kutokana na wivu.

Espérance Ciragane ni mwanachama wa chama cha UNC mjini Bukavu, anasema chama chake pia kimeathirikana anakumbusha kwamba sheria inapiga mafuruku tabia hizo:

Lakini pia, asasi za kiraia jimboni kivu kusini zimewanyooshea kidole cha lawama baadhi ya wagombea ambao hawakusita kubandika picha zao nafasi ambazo hazitakiwi kufanyia siasa kama vile kwenye vibao vya mashule, makanisa, na vibao vya ofisi za taasisi za serikali na kazalika.

Soma pia:Kampeni za uchaguzi mkuu zaanza rasmi Kongo

Mizo Kabare ni msemaji wa uratibu wa shirika la raia wa jimbo la Kivu kusini, anatoa angalizo kwa wagombea nakuitaka tume ya uchaguzi CENI ijihusishe zaidi. Haya yanajiri wakati ambapo hakuna mgombea Urais yeyote aliyekwisha wasili Kivu kusini.

Kati ya wagombea Urais walioanza rasmi Kampeni ya uchaguzi wa desemba 20 mna rais anayemaliza muhula wake wakwanza Felix Tshisekedi anayezunguukakatika majimbo ya magaribi ya Congo, Gavana wa jimbo la zamani la Katanga Moise Katumbi Chapwe aliyeanza kampeni yake upande wa kaskazini mwa Kongo kule Kisangani na ataelekea mjini Goma kabla kuwasili Bukavu jumamosi.

Pia kuna wagombea Uraia Martin Fayulu na Delly Sesanga ambao wameanza kampeni zao katika majimbo ya katikati mwa Congo.

Kumepita wiki moja tangu pale dawati linalosindikiza ugombea Urais wa Daktari Denis Mukwege limetangaza lawama kwamba kwa mara kadhaa utawala umedhidisha njama za kumzuia Mukwege kurejea mjini Bukavu ila hadi hapo mamlaka za Kongo hazikujibu kwa tuhuma hizo.

Vyama vya siasa vya upinzani Afrika vimetekeleza wajibu wao?

02:19

This browser does not support the video element.