SiasaMarekani
Kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yaahirishwa
19 Desemba 2023Matangazo
Mataifa ya Kiarabu yaliyowasilisha kura hiyo wanaitazama hatua hiyo kama ushahidi kwamba Marekani inazidi kukosa subra na mwenendo wa Israel katika ukanda wa Gaza.
Kura hiyo ilipaswa kufanyika jana saa kumi na moja alasiri mjini New York lakini imesogezwa mbele hadi leo.
Hata hivyo, badala ya kupinga tu azimio hilo moja kwa moja kama ilivyofanya awali, vyanzo vimeeleza kuwa Marekani huenda ikakubali "kusimamishwa" kwa mapigano.
Rasimu hiyo imewasilishwa na mataifa ya Kiarabu yakiongozwa na Umoja wa Falme za Kiarabu, na ambayo yametiwa moyo na uungwaji mkono mkubwa wa Umoja wa Mataifa wa kusitisha mapigano wiki iliyopita, wakati nchi wanachama 153 zilipopiga kura ya kuunga mkono azimio lisilo la kisheria la kusitisha mapigano huko Gaza.