1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Kura zaanza kuhesabiwa baada ya uchaguzi wa rais Uturuki

28 Mei 2023

Zoezi kuhesabu kura limeanza muda mfupi uliopita nchini Uturuki baada ya taifa hilo kufanya duru ya pili ya uchaguzi wa rais.

Uchaguzi wa Uturuki
Uchaguzi wa UturukiPicha: Yves Herman/REUTERS

Uchaguzi huo utaamua iwapo rais Reccip Tayyip Erdogan atarefusha muhula wake madarakani au wapiga kura watamchagua kiongozi wa upinzani Kemal Kilicdaroglu

Matokeo ya awali yanatarajiwa kuanza kutolewa jioni hii na wengi wanasubiri kwa shauku kufahamu mwanasiasa atakayejikingia wingi wa kura kupata tiketi ya kuongoza Uturuki kwa miaka mitano ijayo.

Rais Erdogan ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 20 anatazamiwa kuwa na nafasi ya kupata ushindi baada ya kuukosa kwa alama 4 pekee wakati wa duru ya kwanza iliyofanyika Mei 14. Uchaguzi wa leo unatajwa kuwa kipimo cha utawala wa Erdogan anayetuhumiwa na upinzani kwa sera za "mabavu".

Umefanyika ikiwa imepita miezi mitatu tangu kutokea tetemeko kubwa la ardhi nchini Uturuki lililowaua maelfu ya watu na katikati ya mdodoro mkubwa wa kiuchumi kuwahi kushuhudiwa nchini humo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW