Kura zaanza kuhesabiwa katika uchaguzi muhimu wa Taiwan
13 Januari 2024Zoezi la kuhesabu kura limeanza leo kufuatia uchaguzi wa rais na bunge katika kisiwa cha Taiwan, ambao China imeuelezea kuwa ni chaguo kati ya vita na amani.
Soma pia: Mamilioni wapiga kura kumchagua rais na wabunge Taiwan
Uchaguzi huo umefanyika wakati Beijing ikiongeza shinikizo kwa kisiwa hicho kukubali kuwa himaya yake. Matokeo ya uchaguzi wa rais yanapaswa kuwekwa wazi ifikapo leo jioni.
Taiwan imekuwa hadithi ya mafanikio ya kidemokrasia tangu ilipofanya uchaguzi wake wa kwanza wa rais wa moja kwa moja katika mwaka wa 1996, baada ya miongo mingi ya mapambano dhidi ya utawala wa kimabavu na sheria ya kijeshi.
Soma pia: Wafahamu wagombea wakuu watatu wa urais Taiwan
Chama tawala cha Democratic Progressive - DPP, ambacho kinapigania utambulisho wa Taiwan na kinapinga madai ya China kuimiliki ardhi hiyo, kinatafuta muhula wa tatu madarakani. Mgombea wake ni Makamu wa Rais wa Taiwan, Lai Ching-te. Mpinzani wake mkuu Hou Yu-ih anapigia upatu uhusiano na China.