Kura zahisabiwa Jamhuri ya Afrika ya Kati
31 Julai 2023Matangazo
Karibu raia milioni 1.9 walisajiliwa kushiriki kura ya mapendekezo ya mabadiliko hayo yatakayoongeza mamlaka ya rais kutoka muhula wa miaka mitano hadi saba na kuondoa ukomo wa mihula miwili.
Mwaka 2020, Touadera alishinda muhula wa pili hadi mwaka 2025, baada ya uchaguzi kuvurugwa na baadhi ya makundi ya waasi, lakini pia uliokabiliwa na madai ya udanganyifu.
Wapinzani wake sasa wanamshutumu kwamba anataka kuwa rais wa maisha.
Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kutolewa baada ya siku nane.
Mahakama ya katiba inatarajiwa kuchapisha matokeo rasmi Agosti 27.