1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura zahesabiwa Brazzaville, N’Guesso atarajiwa kushinda

16 Machi 2026

Mchakato wa kuhesabu kura unaendelea katika Jamhuri ya Kongo-Brazzaville baada ya kumalizika uchaguzi mkuu uliofanyika jana Jumapili (15.03.2026).

Kongo-Brazzaville  | Denis Sassou Nguesso
Rais wa Kongo-Brazzaville anaetetea kiti chake Denis Sassou N'Guesso.Picha: Russian Foreign Ministry Press Service/TASS/dpa/picture alliance

Rais anaetetea kiti chake Denis Sassou N'Guesso aliyeiongoza nchi hiyo kwa muda mrefu, anawania awamu ya tano. Matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa ndani ya wiki mbili.

Sio watu wengi waliojitokeza kupiga kura, kwa kuwa raia wengi walisema hawaamini uchaguzo huo utaleta mabadiliko ya uongozi kutoka kwa Sassou N'Guesso aliyetawala kwa miaka 42. Kabla ya uchaguzi huo upinzani ulitoa wito kwa raia kuususia.

Wagombea sita walipambana na Sassou N'Guesso mwenye miaka 82 kuwania nafasi hiyo ya juu kwenye moja ya taifa lenye hifadhi kubwa ya mafuta kusini mwa jangwa la Sahara, lakini wachambuzi tayari wamesema hakuna hata mmoja anaetarajiwa kushinda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW