1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kusitishwa msaada wa Marekani kusababisha vifo milioni 14

Josephat Charo
1 Julai 2025

Baada ya shirika la misaada la Marekani USAID kufutwa, nnchi wafadhaili kadhaa wakubwa zikiwemo Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zilifuata mkondo na kutangaza mipango ya kupunguza bajeti zao za misaada ya kigeni.

Kukosekana kwa msaada wa shirika la misaada la Marekani USAID huenda kukasababisha vifo vingi vya ziada kote ulimwenguni
Kukosekana kwa msaada wa shirika la misaada la Marekani USAID huenda kukasababisha vifo vingi vya ziada kote ulimwenguniPicha: DW

Vifo zaidi ya milioni 14 vya ziada, vikiwemo vya watoto milioni 4.5 wenye umri wa chini ya miaka mitano, huenda vikatokea katika kipindi cha miaka mitano ijayo kutokana na kupunguzwa kwa kiwango kikubwa misaada ya kigeni ya Marekani.

Hayo ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa hivi leo na jarida linaloripoti masuala ya afya la Lancet. Utafiti huo ulioongozwa na wanasayansi wa Barcelona na Salvador da Bahia, Brazil, unaonya dhidi ya uamuzi uliochukuliwa na rais wa Marekani Donald Trump wa kupunguza misaada.

Timu hiyo ya wanasayansi ilitathimini data za vifo kutoka zaidi ya nchi na maeneo 130 kati ya mwaka 2001 na 2021, na kuyatumia matokeo ya utafiti huo kubashiri kitakachotokea hadi 2030.

Makadirio yao yanapendekeza kupungua kwa msaada wa Marekani huenda kukawa na athari mithili ya janga, hususan katika nchi za kipato cha kati na cha chini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW