Kutana na Dk. Hawa Abdi: Mwanamke wa shoka Somalia
10 Juni 2011Matangazo
Mara baada ya kumaliza masomo yake ya udaktari, katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev, Dokta Hawa Abdi alirudi Somalia na mwaka 1983 alifungua zahanati yake binafsi kwa ajili ya kutoa huduma ya afya kwa wanawake na watoto. Ni mmoja ya wanawake wa kwanza nchini Somalia kuwa madaktari wanaotibu magonjwa ya wanawake.
Halima Nyanza anaangalia maisha na kazi za mwanamke huyu wa aina yake.