1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUTEULIWA BIBI ANGELA MERKEL KUANIA UKANZELA WA UJERUMANI NA KURA YA MAONI UFARANSA NDIO MADA KUU

31 Mei 2005

Likianzia na kuteuliwa kwa bibi Angela Merkel kuania wadhifa wa ukanzela, gazeti la OSTSEE-ZEITUNG kutoka Rostock laandika:

“Tuliemuona jana, ni bibi Angela Merkel mpya,mwenye bashasha,anaejiamini na ambae aliitikia kama jambo la kawaida uteuzi wake .

Wakati huo huo amepania kutimiza shabaha fulani za kisiasa:Anataka kuwa mtumishi wa kwanza wa nchi hii.Anataka kubadilisha yale yanayoitwa mashirika ya mimi binafsi ambayo hayakuleta faida na maiala pake kuchukuliwa na mashirika ya ‘sisi binafsi”.Bibi Merkel, ambae hadi sasa akikwepa kubainisha wazi wazi mawazo yake,alisisitiza katika hotuba yake kufung amanisha wadhifa wake wa ukanzela endapo akichaguliwa na mabadiliko ya kitamaduni.

Ameelewa kwamba atahatarisha kuchaguliwa kwake endapo akijitokeza kuwa ni mwanasiasa asie na hisia za kuwatetea wanyonge.”-hilo lilikuwa ni OSTSEE-ZEITUNG kutoka Rostock.

Kuteuliwa kwa bibi Medrkel kuania wadhifa wa ukanzela kumekosolewa lakini na gameti la kusini mwa Ujerumani-SÜDDEUTSCHE ZEITUNG.Laandika:

“Siasa zake hadi sasa zazusha shaka shaka kwamba hataki kuweka wazi tangu sasa anachopanga kufanya,lakini siasa hii inajificha nyuma ya boma…… kuwa nchi hii yapasa kujua talari katika kampeni za uchaguzi kwa hatua zipi mtetezi huyu wa ukanzela ana azimia kufufua mfumo wa uchumi wa soko huru.Je, anapanga kupandisha kodi za ununuzi wa bidhaa ?Je, anapanga mageuzi makubwa yak odi ya mapato ?

Akiwa si mwanasiasa maarufu sana, Bibi Angela Merkel aweza kuchaguliwa kuwa Kanzela wa Ujerumani lakini haeezi kuitawala nchi hii kwa njia hiyo.”laandika gameti.

Gameti la WESTDEUTSCHE ZEITUNG linamurika uhusiano kati ya bibi Merkel na mwenyekiti wa chama ndugu cha CSU Bw.Edmund Stoiber:

Gazeti lasema:

“Si sadfta tu kuwa ni bw.Stoiber aliejitokeza katika kizazi hiki kama mkunga .Kwani akiwa kigogo ubavuni mwa Bibi Merkel,atamdhofisha bibi Merkel.Lakini nani ajuwae ? bibi huyu anaweza akageuka baada ya kushinda uchaguzi akampiku hata mwenyekiti huyo wa CSU na kuanza kutamba kuweka nidhamu katika baraza lake la mawaziri….”ni maoni ya WESTDEUTSCHE ZEITUNG.

FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG lina maoni mengine linapoandika:

„Bado bibi Merkel si kanzela wa Ujerumani.Kwa kushinda kuchaguliwa ndani ya chama chake cha CDU na kuuwakilisha baadae muungano wa CDU/CSU kama mtetezi wao wa ukanzela,hakukiuka vizingiti vidogo katika njia yake ya kuparamia ngazi ya ukanzela…..Ikiwa bw.Stoiber wa chama ndugu cha CSU atatekeleza ahadi zake basi itakua taabu kwa muungano wa vyama vya CDU/CSU kushindwa uchaguzi ujao hata ingawa si rahisi kuseleleza maskizano ya hivi sasa baina ya vyama hivyo viwili vya CDU/CSU hadi utakapofanyika uchaguzi.“

Likitugeuzia mada na kutuchukua katika kura ya maoni nchini Ufaransa na kuikataa wapigakura wa huko katiba ya UU-gazeti la COBURGERBLATT, laandika:

„Ah, masikini ulaya.Imesadifu kuwa Ufaransa,muasisi wa UU alieikataa katiba ya Ulaya na pengine kesho wadachi huko Holland watafuata nyayo zao na ,kukataa pia.tangu kupita miaka 50 uinashughulikia amani,usalama na neema na hii ndio shukurani .Si ulaya hii lakini iliokataliwa na wapigakura walioikataa katiba bali umangimeza,hasira kwa kanuni za Umoja huo na nchi zenye ujira wa chini ambazo zinapiga hodi kujiunga na UU na ambazo zitafunguliwa mlango kuingia.Ghadhabu za wapigakura wa Ufaransa zililengwa hasa kwa serikali ya paris.“ni maoni ya TAGEBLATT.

Likitukamilishia, gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU laandika kwa hasira:

„Siasa za Umoja wa Ulaya zinakabiliwa na ajali yake mbaya kabisa na lazima ujue jinsi gani utajiepusha na ajali hiyo.Mvutano uliopo hautokani na bidhaa za kifahari,bali haja ya kuwapo na hakuna njia nyengine ya kuepuka.Na hii inafanya mambo kuwa hata magumu zaidi lakini yaonesha njia ya kunyosha:Kuendelea kuidhinisha katiba ya UU kwa wanachama waliosalia na wakati huo huo kuanzisha mjadala baina ya serikali kuhusu kuhakikisha mageuzi.Kile UU unachohitaji ni mchanganyiko kati ya kuaminika na kuvumbua.“