KUWAIT: Bunge la Kuwait limejiuzulu kuzuia kura ya Jumatatu
4 Machi 2007Matangazo
Serikali ya Kuwait imejiuzulu baada ya kuwa madarakani muda wa miezi minane tu.Wabunge wamesema,lengo ni kuzuia kura ya kutokuwa na imani kupigwa dhidi ya waziri wa afya,Sheikh Ahmad Abdullah al-Sabah.Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya serikali kukosa wingi wa kutosha bungeni,kuweza kuzuia kura iliyopangwa kupigwa siku ya Jumatatu ikiwa na azma ya kumuondoa waziri huyo.