1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuzuka kwa virusi vipya, sababbu ni nini? Ni sisi binadamu?

Angela Mdungu
7 Julai 2020

Virusi vipya vya corona vinahusishwa kuwa vimetokna na Wanyama. Watafiti wanaonya kuwa huenda kuna majanga mengine zaidi ya aina hii. Sababu ni nini? Ni sisi binadamu na matumizi makubwa yasiyo sahihi ya mazingira yetu. 

Australien Corona-Pandemie | Nahrungsverteilung
Picha: Reuters/J. Ross

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa Jumatatu na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP pamoja na taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), magonjwa yatokanayo na wanyama yanatarajiwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kuambukizwa kwa binadamu katika siku zijazo - sawa na kile kilichotokea kwa virusi vipya vya corona.

Katika ripoti hiyo mkuu wa UNEP Inger Anderson ameonya kuwa ikiwa watu wataendelea na matumizi mabaya ya wanyamapori na mfumo wetu wa ikolojia katika mazingira yetu tunaweza kutibua magonjwa yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu katika miaka ijayo.

Mfanyakazi wa afya akiandaa chanjo huko CongoPicha: picture-alliance/AP/S. Mednick

Taarifa ya ripoti hiyo inaonesha kuwa ongezeko kubwa la mahitaji ya nyama, kupanuka kwa miji na mabadiliko ya tabia nchi vyote kwa pamoja yanachangia  katika hili. Hivyo basi ugonjwa wa Covid-19 ni mfano mmoja tu wa ongezeko la magonjwa anayoweza kuambukizwa  binadamu kutoka kwa wanyama. Virusi vya corona vinaaminika kuwa vilitokana na popo na kuwafikia binadamu kupitia wanyama wengine.

Hata virusi vya Ebola navyo vilitokana pia na wanyama, wakati wanyama jamii ya paka wanadhaniwa kuwa walisambaza virusi vya Sars vya mwaka 2003 kwa watu. Delia Randolph, daktari wa mifugo anasema, wakati watu wengi duniani walishangazwa na Covid 19 wao, watafiti wa magonjwa ya mifugo hawakustaajabu.

Anasema ugonjwa huu ni moja kati ya majanga yliyokuwa yakitazamiwa kwa kiasi kikubwa. Anasema  tangu miaka ya 1930 kumekuwa na ongezeko la magonjwa ya binadamu na takribani asilimia 75 ya magonjwa hayo, yanatokana na wanyama wa mwituni. Ripoti hiyo ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo inasema kuwa kuna sababu kadhaa za ongezeko la maradhi hayo yitokanazo na binadamu. 

Mfanyakazi mwingine wa afya akimpima mgonjwa wa COVID-19Picha: Getty Images/AFP/O. Sierra

Katika upande mwingine, maradhi hayo yanasababishwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya protini za wanyama na kukua kwa ufugaji. Matokeo yake ni kwamba kumekuwa na wanyama wengi zaidi wenye mfanano wa kijenetiki ambao wako kwenye hatari ya kupata maambukizi. Pia ripoti hiyo imesema sababu nyingine ni matumizi mabaya ya wanyamapori kupitia uwindaji na biashara pamoja na kuwepo kwa ongezeko la idadi ya watu na kupanuka kwa miji, misitu kukatwa na matokeo yake, watu hujikuta wakisogea karibu zaidi na wanyama. 

Mabadiliko ya tabia nchi yanachochea pia ongezeko la magonjwa. Hali ya joto inaweza kuwa mazingira sahihi kwa vimelea vya maambukizi, inaeleza ripoti hiyo. Mtaalamu wa magonjwa ya mifugo Delia Randolph anaongeza kuwa kupambana na majanga pekee si njia sahihi, kwani ni kama kumtibu mgonjwa kwa kuangalia dalili tu na si chanzo kilichosababisha tatizo. Kwa mujibu wa utafiti, matatizo haya yanahitaji kushughulikiwa ili kuepusha hatari ya magonjwa kama Covid-19