1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwanini Afrika Magharibi inaandamwa na ugaidi?

Angela Mdungu
24 Septemba 2024

Mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye itikadi kali yamezidi kuongezeka katika nchi za Burkina Faso, Mali na Niger. Hivi karibuni kundi la wanamgambo wenye itikadi kali liliushambulia mji mkuu wa Mali.

Viongozi wa kijeshi wa Mali, Niger na Burkina Faso
Viongozi wa kijeshi wa Mali, Niger na Burkina Faso Picha: Mahamadou Hamidou/REUTERS

Hivi karibuni kundi la wanamgambo wenye itikadi kali liliushambulia mji mkuu wa Mali. Lilifanikiwa kuondoka mjini hapo bila kugunduliwa muda mfupi kabla ya sala ya adhuhuri. Wanamgambo hao waliwauwa makumi ya wanafunzi katika kituo cha mafunzo ya polisi na kuvamia uwanja wa ndege wa Bamako. Zaidi ya hapo, waliichoma moto ndege ya Rais.

Tukio hilo la Septemba 17 lilikuwa baya zaidi kuwahi kufanywa katika mji mkuu kwenye Ukanda wa Sahel tangu mwaka 2016. Shambulio hilo lilionesha kuwa makundi yenye itikadi kali yaliyo na uhusiano na al Qaeda au kundi linalojiita dola la Kiislamu yanaweza pia kushambulia hata yalipo makao makuu ya dola.Jeshi la Mali ladhbiti hali Bamako kufuatia shambulizi

Wakati mgogoro huo wa Ukanda wa Sahel ukifunikwa  na vita vya Sudan na Mashariki ya Kati, ni wazi kuwa unachangia pakubwa ongezeko la wahamiaji kutoka kanda hiyo kuelekea Ulaya. Hili linaendelea wakati vyama vinavyopinga wahamiaji vinavyofuata siasa kali za mrengo wa kulia vikizidi kuongezeka na mataifa ya Umoja wa Ulaya yakiimarisha mipaka yao.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM, njia ya kuelekea Ulaya inayotumiwa zaidi kwa mwaka huu ni kupitia Pwani ya nchi za Afrika Magharibi kuelekea visiwa vya Kanari huko Uhispania.

Jeshi la Mali ladhibiti usalama baada ya shambulio Bamako

01:43

This browser does not support the video element.

Data za Shirika hilo zinaonesha kuwa idadi ya wahamiaji wanaowasili Ulaya kutoka Burkina Faso, Chad Mali, Mauritania, Niger, Nigeria na Senegal ilipanda hadi watu 17,300 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu kutoka wahamiaji 10,000 mwaka uliopita.

Umoja wa Mataifa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji yameelekeza lawama zao kwa mzozo wa Sahel na mabadiliko ya tabianchi kuwa ndivyo vilivyosababisha ongezeko hilo la wahamiaji.jeshi la Marekani lamaliza kuondoka Niger, baada ya mchakato ulioanza tangu ilipotakiwa kuondoka

Wanadiplomasia 15 na wataalamu wanasema kuwa sehemu kubwa ya eneo linalodhibitiwa na makundi yenye itikadi kali sasa yanakuwa maeneo ya mafunzo na ya kufanyia mashambulizi makubwa kuelekea miji muhimu kama vile Bamako au nchi jirani na miundo mbinu ya mataifa ya magharibi yaliyo ndani ya kanda hiyo au kwingineko.

Vurugu zinazofanywa na makundi hayo na hasa madhara makubwa yaliyovisababishia vikosi vya serikali ilikuwa sababu kubwa ya wimbi la mapinduzi ya kijeshi tangu mwaka 2020 dhidi ya serikali za Burkina Faso, Mali na Niger, zilizokuwa zikiungwa mkono na mataifa ya magharibi.

Wawakilishi wa kijeshi wa MaliPicha: AP/picture alliance

Mataifa hayo ya magharibi ambayo awali yaliwekeza katika kuyashinda makundi ya itikadi kali , kwa sasa yana uwezo mdogo katika maeneo hayo hasa tangu watawala wa kijeshi wa Niger walipoiamuru Marekani iondoe vikosi vyake katika kambi ya droni ya Agadez.

Wanajeshi wa Marekani na Shirika lake la Kiitelijensia la CIA lilikuwa likitumia droni kuwafuatilia wanamgambo na kutoa taarifa kwa washirika wake kama vile Ufaransa ambao walifanya mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo hao.

Soma: Mali, Burkina na Niger kuanzisha pasi mpya za kusafiri za bayometriki

Wamarekani walifukuzwa nchini humo baada ya kukataa kuwapa watawala wa kijeshi taarifa za kiitelijensia na kuwatahadharisha dhidi ya kufanya kazi na Warusi.

Uchambuzi wa data za shirika linalofuatilia migogoro la (ACLED) ullibaini kuwa, idadi ya matukio ya vurugu yanayoyahusisha makundi ya wanamgambo  katika nchi za Sahel yameongezeka mara mbili tangu mwaka 2021

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Kumekuwa na wastani wa mashambulio 224 kwa mwezi  kutoka 128 mwaka 2021. Moja ya masuala yanayoyapa wasiwasi mataifa ya Magharibi ni uwezekano wa Sahel kugeuka kuwa ngome kuu ya makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu kama ilivyo kwa Afghanistan au ilivyokuwa Libya kipindi cha nyuma.