1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wamarekani zaidi wenye asili ya Asia wanunua silaha

16 Novemba 2023

Wamarekani wenye asili ya Asia wanamiliki silaha kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na raia wengine. Lakini ongezeko la mashambulizi ya kibaguzi na uhalifu vinazidi kuondoa imani yao katika mfumo wa sheria wa Marekani.

Marekani| Arcadia Firearm & Safety
David Liu ndiye mmiliki wa duka la kuuza silaha la Arcadia Firearm & Safety mjini CaliforniaPicha: Leah Carter/DW

Duka la bunduki la David Liu linaonekana kutotia wasiwasi kutoka nje. Akiwa nyuma ya jumba tulivu la maduka mjini Arcadia, karibu na Los Angeles, Liu anaweka kibao cha juu cha mgahawa wa sushi ambao hapo awali ulikuwa na duka lake la ukubwa wa sebule. Anafanya hivyo ili kusalia siri, akisema watu wanaohitaji kumpata watamtafuta.

Liu anaweka vipeperushi kwenye madirisha yake vinavyotoa madarasa juu ya leseni za silaha za siri, kwa Kimandarin na Kiingereza, na kubandikwa chini ya bendera yake ya Trump 2020, okidi na samaki wa mapambo. Liu anasema takriban nusu ya wateja wake ni Waasia - hasa Wachina - na wanafanya miamala katika lugha yao ya asili.

Soma pia: Marekani: Idadi ya visa vya watu kujiua yaongezeka

Wateja wake wengi kwenye duka lake ni kama marafiki - watu wa kawaida wanaokuja kwa vipindi vingi vya mafunzo, kazi za kiofisi, au kuzungumza. Baadhi yao ni wamiliki wapya wa bunduki wanaotokana na hofu juu ya kuongezeka kwa viwango vya vurugu na uhalifu wa chuki, ambao uliongezeka kwa zaidi ya asilimia 330 kati ya 2020 na 2021, kulingana na ripoti ya Kituo cha Utafiti wa Chuki na Misimamo Mikali iliyochapishwa mwaka 2022.

Arcadia ni eneo lenye wakazi wengi wa Asia dakika chache tu kutoka Monterey Park, eneo la shambulizi baya la risasi lilifuatia Tamasha la Mwaka Mpya mwaka huu.

Mlipuko wa UVIKO-19 ulisababisha mashambulizi dhidi ya Waasia wa MarekaniPicha: Ben Gray/dpa/AP/picture alliance

Ongezeko la wamiliki wa bunduki

Wamarekani wenye asili ya Asia kawaida huwa na viwango vya chini zaidi vya umiliki kuliko jamii yoyote nchini Merika, lakini walishuhudia ongezeko la umiliki kwa asilimia 43 kati ya 2019 na 2020, kuanzia na janga. Mlipuko wa COVID-19 uliripotiwa kuchochea unyanyasaji wa umma wa Waasia nchini Marekani. Uhalifu kama vile uporaji na wizi wa nyumba pia umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni kufuatia janga hili na kupanda kwa kasi kwa gharama ya maisha.

Soma pia: Biden ataka silaha za mashambulizi zipigwe marufuku

Liu anasema kuwa katika eneo la Los Angeles, Wachina wakati mwingine wanalengwa kwa vurugu hadharani na majumbani mwao kutokana na dhana potofu ya kuhifadhi kiasi kikubwa cha fedha taslimu.

"Hali inazidi kuwa mbaya," anasema Ray Gong, 27, mteja wa Liu. "Nimetoka tu jeshini hivi karibuni, na baada ya kusikia habari hizi, mawazo yangu yakabadilika."

Gong aliwasili Marekani mwaka 2016 kutoka Hangzhou, mji wa mashariki nchini China kusini mwa Shanghai. Alinunua bastola yake ya kwanza mwezi Agosti na bunduki nyingine mbili mwezi Septemba, akitarajia "kuwa tayari kwa lolote."

Anasema licha ya kuwa hajawahi kukumbana na vurugu zinazohusiana na kabila lake, alibaguliwa katika jeshi, ambapo alizuiwa kuchukua nafasi za juu kutokana na kuwa Mchina na mara nyingi alikabidhiwa kazi ambayo hakuna mtu mwingine aliitaka.

Pia yuko katika harakati za kupata leseni yake ya ubebaji wa silaha, ambayo kwa kawaida huchukua zaidi ya miezi sita huko California. "Ninafikiria kuibeba (bunduki) kila wakati."

Gong sasa ni mwanachama wa kundi la mazoezi ya upigaji bunduki lililoko karibu, na anasema anafanya kazi kwenye mazoezi ya kulenga shabaha angalau mara moja kwa wiki.

Ray Gong, mteja wa Arcadia Firearm & Safety, hufanya mazoezi y akupiga bunduki katika eneo la La Puente Picha: Leah Carter/DW

Katika uchunguzi wa Taasisi ya Sera ya Umma ya California mwaka jana, thuluthi mbili ya Wakalifornia waliutaja uhalifu kama tatizo kubwa.

Soma pia:Biden aomboleza mauaji ya kutumia bunduki huko Texas 

"Kila mtu (sio Waamerika wa Asia pekee) wananunua bunduki zaidi," anasema Liu. "Watu wanaogopa."

Ricky Wong, mwenye umri wa miaka 44, msimamizi wa sheria, anasema kwamba katika miaka michache iliyopita, alinusurika kushambuliwa kwa kutumia mpira wa besiboli na wizi wa magari mawili. Shambulio hilo, alisema, lilitekelezwa na Waasia wengine. Hapo awali alikuwa mmiliki wa bunduki, lakini shambulio hilo na ujambazi vilithibitisha uamuzi wake wa kuwa na silaha.

Wito kwa mfumo wa haki kuimarishwa kukabiliana vyem dhidi ya vurugu

Mojawapo ya suluhu la kuongezeka kwa uhalifu wa kutumia nguvu huko California, Wong na Liu wanasema, ni kukabiliana na uhalifu tena, wakitaja wauaji wengi ambao waliachiliwa huru baada ya kile wanachoona kama kifungo cha muda mfupi sana gerezani.

Chris Cheng, mpiga risasi na mwanachama mwanzilishi wa Jumuiya ya Wamiliki wa Bunduki wa Amerika, Pasifiki na Asia, aliunga mkono maoni kwamba utekelezaji wa sheria haushughulikii kikamilifu uhalifu wa vurugu.

"Kukosekana kwa mashtaka" na mawakili wa wilaya katika miji mikubwa, ikiwa ni pamoja na Los Angeles na nyumbani kwake, San Francisco, dhidi ya wahalifu wanaoendesha mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya Waasia kulipunguza imani ya jumuiya hiyo katika mfumo wa haki ya jinai.

Raia wa marekani wanaongoza kwa kumiliki bunduki duniani

00:53

This browser does not support the video element.

Soma pia: Trump kuwapa bunduki waalimu

"Ukichanganya kwamba pamoja na kuongezeka kwa ghasia za wenyewe zilizosababisha na mauaji ya George Floyd na uasi wa Januari 6, haipaswi kushangaza kwamba Wamarekani wengi wenye asili ya Asia walianza kuelewa kwamba mfumo wa sheria hauwezi kuwalinda."

Hata hivyo, si kila mtu anahisi kwamba silaha za moto si jibu la kuongezeka kwa uhalifu wa chuki. "Sekta ya silaha na ushawishi wa bunduki kwa sasa vinalenga jumuiya za wachache katika uuzaji wao katika kukabiliana na vilio vya muda mrefu katika soko la bunduki la watu weupe," kulingana na ripoti iliyotolewa na Kituo cha Sera ya Unyanyasaji chenye makao yake makuu mjini Washington.

"Kutokana na kuongezeka kwa wingi wao na nguvu ya ununuaji, Wamarekani wenye asili ya Asia wanatazamwa kama soko ambalo halijatumiwa na watengenezaji bunduki," ilisema ripoti hiyo.

Liu anaiona motisha ya wateja wake sio kama matokeo ya masoko bali ni matokeo ya hofu. "Ni hatari sana huko nje. Watu wengi wanaonunua ni waathirika tayari."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW