1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Kyiv: Urusi imeshambulia kituo cha treni kilichofurika watu

27 Desemba 2023

Ukraine imesema vikosi vya Urusi vimekishambulia kwa kombora kituo kimoja cha treni kwenye mji wa Kherson wakati mamia ya watu walikuwa wakisubiri usafiri ili kutoroka mapigano.

Mapigano vita vya Urusi na Ukraine.
Mapigano vita vya Urusi na Ukraine.Picha: Alexander Polegenko/TASS/dpa/picture alliance

Waziri mambo ya ndani wa Ukraine, Ihor Klymenko, ameandika kupitia ukurasa wa mtandao wa Telegram kwamba afisa mmoja wa polisi ameuwawa na wengine wawili wamejeruhiwa kwenye shambulio hilo.

Amesema hivi sasa zaidi ya watu 100 wanapangiwa kuondoka eneo hilo kwa kutumia mabasi kupelekwa eneo salama. Mji wa Kherson uliangukia mikononi mwa Urusi katika siku za mwanzo za vita lakini ulikombolewa na vikosi vya Ukraine miezi michache baadaye.

Unapatikana kwenye jimbo la kusini mwa Ukraine lenye jina sawa na hilo na ambalo Urusi ilidai kulikamata mwaka uliopita licha ya ukweli kwamba hadi sasa bado imeshindwa kuchukua udhibiti kamili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW