1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Historia

Léopold Senghor: Mfungwa aliyekuja kuwa rais

Yusra Buwayhid
13 Februari 2020

Léopold Sédar Senghor anachukuliwa kama mmoja wa viongozi na wasomi wakuu wa Afrika, mwandishi na mshairi. Baada ya kufungwa jela wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, alikuja kuwa Rais wa kwanza wa Senegal.

Léopold Senghor: Mfungwa aliyekuja kuwa rais

02:10

This browser does not support the video element.

 

Vipi maisha ya Léopold Sédar Senghor yanaweza kuelezewa kwa ufupi?

Alizaliwa Oktoba 9, 1906, kusini-mashariki mwa mji mkuu wa Dakar nchini Senegal. Senghor alikuwa mwanzilishi na mtetezi wa Négritude, vuguvugu la harakati za kisiasa na za uandishi liloanzishwa miaka ya 1930. Alikuja kuwa Rais wa Jamhuri ya Senegal mnamo Septemba 1960, baada ya kufanya kazi kama mwandishi wa habari, miongoni mwa mambo mengine. Alisalia kuwa kiongozi wa taifa hilo kwa miongo miwili. Alifariki mnamo Desemba 20, 2001, akiwa na miaka 95, nchini Ufaransa.

Kipi muhimu cha kukumbukwa kuhusu Léopold Sédar Senghor?

Léopold Sédar Senghor alikuwa mtu anayependa amani, ubinadamu, na katika kazi yake alikuwa ni mwenye kuamini juu ya kutenda jambo kwa ukamilifu wake. Alikuwa msomi mwenye kupenda sana kujifunza lugha tofauti. Mnamo mwaka 1984, alikuwa ni mwandishi wa kwanza mweusi kuchaguliwa kama mwanachama wa Académie française - baraza maarufu la lugha Ufaransa. Bila ya pingamizi, alikuwa ni kiongozi wa kwanza barani Afrika kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe bila shinikizo la umma.

Léopold Senghor: Mfungwa aliyekuja kuwa rais

This browser does not support the audio element.

Ni misemo gani ya Léopold Sédar Senghor ambayo bado inakumbukwa?

"Hisia inalingana na mtu Mweusi kama, ilivyo hoja kwa lugha ya Kigiriki". Licha ya ukosoaji ilomkabili, hakuwahi kukana umuhimu wa hisia kwenye suala la uandishi. Aliwakemea wapinzani wake kwa kutokujaribu kuelewa umuhimu wake.

"Staarabika na usistaarabishwe". Kupitia nukuu hii na nyingine nyingi maarufu, Senghor anamhimiza kijana wa Kiafrika kujifunza kila kitu kinachotokana na tamaduni ya zamani na kujiongezea maarifa hayo ya tamaduni kwa upana zaidi kitu ambacho kilikuwa hakiwezekani kwa watu wa jamii ya zamani.

"Ustaarabu wa Ulimwengu". Maneno hayo yanatokana na nadharia maarufu ya Senghori ya ustaarabu na uwazi, wa kutoa na kupokea. Inaelezea mchanganyiko wa mtu mweusi na lugha ya Kigiriki utakaozaa "Mtu Mpya Mweusi", mtu kamili na mwenye kizazi kikubwa.

Asili ya Afrika | Léopold Sédar Senghor

Ni makosa gani yaliyoathiri maisha ya Senghor?

Kati ya mwaka 1962 na 1968, Léopold Sédar Senghor  alifanya makosa kadhaa ya kisiasa wakati akijaribu kulinyamazisha vuguvugu la Popular Front la nchini Senegal. Mwaka 1968 alikabiliana na kundi la wasomi la vuguvugu lilokuwa likifuata muongozo wa  Marxism, mwanafalsafa mzaliwa wa Ujerumani wa karne ya 19 ambaye kazi zake zilihusisha nadharia za kiuchumi, sosholojia na siasa na baadae zilikuja kubadili siasa katika mataifa mengi duniani.

Léopold Sédar Senghor alienziwa vipi?

Senghor alitunukiwa tuzo nyingi za heshima, miongoni mwao ni 'French Legion of Honor' ambayo ni tuzo ya heshima kubwa ya nchini Ufaransa, mwaka 1968 alipewa Tuzo ya Amani ya Uandishi wa Vitabu Ujerumani, na alitunukiwa shahada kadhaa kutoka Vyuo Vikuu maarufu duniani kote. Taasisi kadhaa zimepewa jina lake, ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Léopold Sédar Senghor, uwanja wa mpira na uwanja wa ndege Senegal; Chuo Kikuu cha Senghor cha lugha ya Kifaransa mjini Alexandria nchini Misri; na Taasisi ya Senghor nchini Ureno.

Ushauri wa kisayansi kuhusu makala hii umetolewa na wanahistoria Profesa Doulaye Konaté, Lily Mafela, Ph.D., na Profesa Christopher Ogbogbo. Mfululizo wa makala za Asili ya Afrika umefadhiliwa na Taasisi ya Gerda Henkel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW