La Paz. Waandamanaji wa Bolivia wamtaka kiongozi wa mpito kutaifisha haraka biashara ya gesi ama sivyo wataingia tena mitaani.
11 Juni 2005Matangazo
Waandamanaji wa Bolivia wamemuonya kiongozi wao wa mpito nchini humo kuwa wataingia tena mitaani iwapo hatashughulikia haraka utaifishaji wa biashara ya gesi ya asili.
Onyo hilo limekuja wakati kiongozi wa mahakama kuu Eduardo Rodriguez alipochukua madaraka ya urais toka kwa Carlos Mesa na kuahidi uchaguzi kabla ya mwishoni mwa mwaka huu katika juhudi za kumaliza hali ya ghasia.
Mesa alikuwa rais wa pili katika kipindi cha miezi 20 kulazimika kujiuzulu baada ya maandamano yaliyofanywa na watu wa asili ya nchi hiyo Wahindi kwa muda wa wiki kadha wakidai kupata sehemu kubwa ya utajiri wa nchi hiyo wa mali asili ya nishati.