1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Labor yashinda uchaguzi mdogo wa Uingereza

3 Mei 2024

Chama tawala nchini Uingereza, Conservative, kimeshindwa kutetea kiti cha ubunge mbele ya chama kikuu cha upinzani cha Labour, wakati taifa hilo likisubiri matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa

Uingereza
Labor yashinda uchaguzi mdogo wa Uingereza Picha: Jessica Taylor/AFP

Chama cha Labour kimejinyakulia jimbo la Blackpool Kusini kwa asilimia 26.3 na mgombea wake, Chriss Webb ameuita ushindi huo kuwa ujumbe kwa Conservative:

"Watu wa Blackpool Kusini wamezungumza kwa ajili ya Uingereza. Wamemwambia Rishi Sunak na Conservatives imetosha. Wamechoshwa na miaka 14 ya Conservatives kuwa madarakani, wamepoteza imani ya Waingereza. Na Blackpool nayo imechoshwa na hii serikali iliyoshindwa na kuharibu uchumi, huduma zetu za umma na kuongeza kodi. Wamesema ni wakati wa mabadiliko - na mabadiliko yameanzia hapa Blackpool usiku wa leo."

Labour yashinda viti vya ubunge katika ngome ya Conservative Uingereza

Matokeo ya awali yalionesha Labour inaweza kushinda viti vingi vya udiwani, lakini macho yote yalikuwa kwenye kinyang'anyiro cha mameya wa mikoa na wa mji mkuu, London, ambapo matokeo yanatarajiwa kutoka baadaye leo ama kesho Jumamosi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW