Lagos.Mahakama: Makamu wa rais Nigeria ruksa kugombea urais:
17 Aprili 2007Matangazo
Mahakama kuu ya Nigeria imetoa uamuzi kuwa tume ya uchaguzi nchini humo imemuengua makamu wa rais wa nchi hiyo Atiku Abubakar kinyume na sheria katika kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao.
Tume hiyo ya uchaguzi hapo mapema ilimuondoa Abubakar kutoka katika orodha ya wagombea kutokana na utata juu ya kushtakiwa kwake kwa madai ya kughushi.
Hatua hii inasafisha njia kwa Abubakar kugombea katika uchaguzi wa rais utakaofanyika siku ya Jumamosi.
Wakati huo huo chama tawala cha Peoples Democratic kimetangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika siku ya Jumamosi kwa ajili ya wabunge wa majimbo na magavana.
Makundi ya haki za binadamu na upande wa upinzani umeueleza uchaguzi huo kuwa ulikuwa na udanganyifu wa hali ya juu.