1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Lai: China kamwe haiwezi kuiwakilisha Taiwan

10 Oktoba 2024

China haina haki ya kuiwakilisha Taiwan, ila kisiwa hicho kiko tayari kushirikiana na Beijing kukabiliana na changamoto kama mabadiliko ya tabia nchi.

Lai Ching-te | taiwanesischer Präsident
Rais wa Taiwan Lai Ching-tePicha: Ann Wang/REUTERS

Haya ni kulingana na Rais wa Taiwan Lai Ching-te siku ya Alhamis huku hiyo hatua yake ya kuonekana kuuma na kuvivia ikiighadhabisha China.

Lai aliyeingia afisini mwezi Mei baada ya kuchaguliwa mwezi Januari, haungwi mkono na China ambayo inamuita "mtenganishi". Beijing inadai kuwa Taiwan ambayo ina utawala wa kidemokrasia iko chini ya himaya yake, mtazamo ambao Lai na serikali yake wanaukataa.

Akitoa hotuba muhimu ya taifa nje ya afisi ya rais mjini Taipei, Lai amesisitiza kwamba Jamhuri ya China - ambalo ndilo jina rasmi la Taiwan, na Jamhuri ya Watu wa China, hazitegemeani.

Ukanda wa TaiwanPicha: Chinese People's Liberation Army/Anadolu/picture alliance

"Katika ardhi hii, demokrasia na uhuru vinakuwa na kustawi. Jamhuri ya Watu wa China haina haki ya kuiwakilisha Taiwan," alisema Lai.

Azma ya taiwan kutetea uhuru wake, kudumisha amani katika Ukanda wa Taiwan na kutafuta mazungumzo ya usawa na heshima na China, hivyo bado havijabadilika, aliongeza Lai.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW