Lai Ching-te aapishwa rasmi kuwa rais mpya wa Taiwan
20 Mei 2024Taiwan imemwapisha Lai Ching-tekuwa rais mpya wa kisiwa hicho katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa wa kimataifa. Lai, ambaye amewahi kushikilia nafasi ya makamu wa rais chini ya rais anayeondoka Tsai Ing-wen, amekula kiapo leo katika ofisi ya rais na kisha kufuatiwa na uapisho wa naibu wake Hsiao Bi-khim.
Lai, anaingia madarakani, mnamo wakati China ikizidisha shinikizo la kijeshi na kisiasa dhidi ya kisiwa hicho kinachojitawala. China inadai kwamba Taiwan ni sehemu ya himaya yake na imemtaja Lai kuwa "mtu hatari anayetaka kujitenga" na ambaye atasababisha mvurugano dhidi ya kisiwa hicho.
Kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Ing-wen, Lai ni mtu anayepigia upatu demokrasia ya kisiwa hicho na katika kipindi cha nyuma amewahi kujinasibu kama mtu wa vitendo katika uhuru wa Taiwan.