1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Laura Bush ziarani Zanzibar

14 Julai 2005

Zanzibar:

Mke wa Rais George Bush wa Marekani, Laura Bush, leo ameitembelea Zanzibar. Ametembelea madrasa na Shule ya ualimu kabla ya kuelekea Kigali, Rwanda ambako ataandamana na Mke wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Cherie Blair. Ulinzi ulikuwa mkali kutokana na ukweli kuwa ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam ulishambuliwa kwa mabomu wakati mmoja na ule wa Nairobi, Kenya na Magaidi wa Al-Qaida mwaka 1998. Bibi Bush jana alikuwa mjini Dar es Salaam, ambako ameahidi kutoa msaada wa Dollar 500,000 kwa lengo la kuunga mkono Mpango wa Kanisa Katoliki wa kuwasaidia Wagongwa wa UKIMWI na virusi vyake na familia zao. Ziara ya Bibi Bush, ambaye anaandamana na Binti wake wawili, inajishughulisha zaidi na masuala ya elimu, UKIMWI na virusi vyake na kuwapatia madaraka akina mama. Bibi Bush, ameondoka Zanzibar na kuelekea Kigali, Rwanda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW