1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Lavrov aanza ziara Afrika kwa kuitembelea Guinea

3 Juni 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amewasili hii leo nchini Guinea, katika ziara ya kwanza ya mwanadiplomasia wa ngazi za juu wa Moscow nchini humo tangu mwaka 2013.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei LavrovPicha: Vyacheslav Prokofyev/dpa/TASS/picture alliance

Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imetangaza ziara hiyo kupitia mtandao wa Telegram, na kuchapisha picha ya Lavrov akiwa katika uwanja wa ndege wa Conakry, ingawa haikueleza zaidi juu ya ziara hiyo.

Shirika la habari la serikali, Tass lilisema tu kwamba Guinea itakuwa sehemu ya ziara ya Lavrov barani Afrika, lakini halikutaja mataifa atakayoyatembelea.

Shirika jingine la habari la Urusi la afrinz.ru lilisema Lavrov anakwenda Chad siku ya Jumatano akiongoza ujumbe muhimu na huenda pia akazuru Burkina Faso.

Mwezi Julai mwaka jana, Rais Vladimir Putin wa Urusi, aliwakaribisha viongozi wa Afrika kwenye mkutano wa kilele mjini Saint Petersburg na kusema walikubaliana kuhamasisha msingi wa kilimwengu unofuata mifumo mingi na kupambana na ukoloni mamboleo.