1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Lavrov ahudhuria mkutano wa Caucasus nchini Iran

Josephat Charo
24 Oktoba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov amefanya mazungumzo na mawaziri wenzake katika mji mkuu wa Iran, Tehran, kuhusu hali katika eneo la Caucusus Kusini.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei LavrovPicha: Vyacheslav Prokofyev/dpa/TASS/picture alliance

Sergei Lavrov pia alifanya mazungumzo tofauti na waziri wa mambo ya nje wa Iran, Hussein Amirabdollahian. Mkutano huo wa ngazi ya mawaziri ulilenga kuzijumuisha jamhuri tatu za zamani za muungano wa zamani wa Sovieti katika eneo la Caucusus, zikiwamo Armenia, Azerbaijan na Georgia, pamoja na dola kubwa jirani - Urusi, Uturuki na Iran.

Georgia iliamua kutoshiriki mkutano huo wa pande sita. Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni hali kufuatia harakati za Azerbaijan katika eneo la Nagorno-Karabakh na kutimuliwa kwa Warmenia kutoka eneo hilo. Mzozo kati ya Azerbaijan na Armenia haujatatuliwa kikamilifu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW