Lavrov azuru Eritrea
27 Januari 2023![Minister Sergey Lavrov trifft Esteban Lazo Hernandez](https://static.dw.com/image/63958108_800.webp)
Matangazo
Lavrov ambaye yuko katika ziara yake ya pili barani Afrika katika kipindi cha miezi sita, alikutana na Rais Isaias Afwerki.
Waziri wa Habari wa Eritrea, Yemane G. Meskel, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba majadiliano yao yaliangazia mwenendo wa vita vya Ukraine na kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili katika sekta ya nishati, madini, teknolojia ya habari, elimu na afya.
Ziara ya Lavrov kwenye bara la Afrika, ambalo limegawika tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, imemfikisha pia Angola, Eswatini na Afrika Kusini.