Lavrov: Urusi haitoshindwa vita nchini Ukraine
6 Desemba 2024Matangazo
Ameyasema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na mwandishi wa habari wa Marekani Tucker Carlson yaliyochapishwa jana Alhamisi.
Katika mahojiano hayo yaliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya X na YouTube, Lavrov amesema lazima Marekani na washirika
Urusi yasema iko tayari kwa lolote vita vya Ukraine
wake ambao wanaipa Ukraine silaha waelewe kwamba, Urusi iko tayari kutumia njia zozote zile kuhakikisha kwamba Marekani na washirika wake, hawatafanikiwa katika kile walichokiita "kushindwa kimkakati kwa Urusi."
Mwanadiplomasia huyo ameongeza kuwa Urusi inapigania maslahi ya usalama wake.