Lavrov ziarani Malta
5 Desemba 2024Matangazo
Ikiwa ziara yake ya kwanza kwenye taifa mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu kuanza kwa vita vya Ukraine, Lavrov aliwasili kwenye mji mkuu wa Malta, Valletta, hapo kwa jana kwa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa kigeni wa jumuiya hiyo.
Picha za vidio zilimuonesha waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Urusi akiwasili kwa ndege ya nchi yake, ingawa ndege za Urusi zimepigwa marufuku kwenye anga la Umoja wa Ulaya.
Soma zaidi: Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi yuko ziarani Cairo
Hata hivyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi, Maria Zakharova, amezuiwa kumsindikiza Lavrov, baada ya viza yake kufutwa na Malta muda mfupi kabla ya kuondoka Moscow.