Wabunge wa Lebabon wahuzuria kikao licha ya maandamano
11 Februari 2020Watu wasiopunguwa 280 wamejeruhiwa leo mjini Beirut kufuatia maandamano ya kujaribu kuzuiya bunge la nchi hiyo kupiga kura ya kuidhinisha serikali mpya. Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi karibu na majengo ya bunge ambako shirika la msalaba mwekundu limesema zaidi ya waandamanaji 39 walilazwa hospitalini kufuatia majiraa. Hata hivyo kikao cha bunge kiliendelea.
Mamia ya wandamanaji walijitokeza leo mjini Beirut mbele ya bunge la nchi hiyo katika juhudi za kuwazuwiya wabunge kutoipigia kura ya imani serikali mpya ya waziri mkuu Hassan Diab.
Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na maji ya moto ilikuwatawanya wandamanaji ambao walirusha mawe kwenye magari ya mawaziri na wabunge waliohudhuria kikao hicho.
Kuna umuhimu wakueko muungano wa raia wa Lebanon
Wandamaniji hao wanaipinga serikali ya waziri mkuu mpya kwa kile wanacho elezea kwamba haitokelezi madai yao.
Baadhi ya wabunge walilala bungeni kwa hofu kwamba idadi ya wabunge wanaohitajika haitokamilika ili kufanikisha kuidhinishwa serikali hiyo mpya kama ilivokuwa kwenye vikao vilivyopita.
Mbunge wa chama cha AMAL kinachoungwa mkono na washia nchini humo, Kassem Hashem amesema kwamba kuna umuhimu wa kuweko na muungano wa raia wa Lebanon ilikutafuta ufumbuzi wa mzozo huo:
'' Tuseme kwa uwazi mzozo huu haukomei kwa serikali au kambi ya kisiasa au kwa kundi ndani ya bunge. Tunakabiliwa na mzozo mbaya kabisa na tunapaswa kuunganisha juhudi zetu zote kuutatua vinginevyo tutaitumbukiza nchi yetu kwenye taathira kubwa sana.''
Wabunge 68 miongoni mwa 128 wa bunge la nchi hiyo kikao cha leo. Kwenye mtandao wa twita,jeshi lilitahadharisha wanadamanaji kwa kile ilichoelezea kueko na visa vya uharibifu ambavyo vinayapa kisogo madai yao ya mwanzo.
Juma tatu polisi walifunga barabara zote zinazoelekea Nijmeh Square ambako bunge la libanon linakopatikana.
Uchumi wa Lebanon wadidimia
Januari 21,waziri mkuu mpya Hassan Diab aliunda baraza jipya la mawaziri 20 ambalo lengo lake ni kukabiliana na tatizo mbaya kabisa la kiuchumi linaloikumba nchi hiyo ya mashariki ya kati toka miaka ya 75 na 90.
Wandamanaji walipinga uteuzi wa Diab kama waziri mkuu kwa sababu anaungwa mkono na kundi la Hezbollah na mshirika mkuu wa rais wa nchi hiyo Michel Aoun.
Licha ya ahadai za waziri mkuu la kuyampa ufumbuzi madai ya waandamanaji,lakini serikali hiyo iliundwa kwa mfumo wa vyama vya kisiasa na makundi ya kidini.Badala ya wanasiasa ,waandamani walikuwa wakidai kueko na serikali ya wataalamu.
Toka oktoba mwaka jana maandamano yalizuka nchini Libenano kwa kupinga siasa ya nchi hiyo ambayo wandamanji waliita kuwa ya rushwa na wasiomudu.