1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lebanon yaituhumu Israel kwa kukataa usitishwaji mapigano

1 Novemba 2024

Waziri Mkuu wa Lebanon ameituhumu Israel kwa kuukataa mpango wa kusitishwa mapigano kati yake na Hezbollah. Hii ni baada ya jeshi la Israel kuilipua ngome ya Hezbollah kusini mwa Beirut kwa mara ya kwanza wiki hii.

Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati
Waziri Mkuu wa Lebanon Najib MikatiPicha: Mohamed Azakir/REUTERS

Waziri Mkuu wa Lebanon ameituhumu Israel kwa kuukataa mpango wa kusitishwa mapiganokati yake na Hezbollah. Hii ni baada ya jeshi la Israel kuilipua ngome ya Hezbollah kusini mwa Beirut kwa mara ya kwanza wiki hii. Waziri Mkuu Najib Mikati amelaani kile alichokiita "utanuzi" wa mashambulizi ya Israel, akisema yanaashiria kukataa kwake kushiriki katika mazungumzo ya kuweka chini silaha.

Karibu mashambulizi 10 ya kutokea angani yalivipiga vitongoji vya kusini kabla ya alfajiri leo baada ya Israel kutoa maagizo ya kuwataka wakaazi wahame. Mashambulizi hayo yamejiri siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kukutana na maafisa wa Marekani kujadili uwezakano wa makubaliano ya kumaliza vita nchini Lebanon, kabla ya uchaguzi wa rais Marekani Jumanne ijayo.Lebanon yahitaji msaada wa jumuiya ya kimataifa kujiimarisha

Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Israel katikati mwa Gaza yamepanda hadi watu 25, wakiwemo watoto watano. Maafisa wamesema watu 13 waliuawa leo katika mashambulizi ya angani nchini Lebanon. Watu 16 walikuwa wameripitiwa kuuawa katika mashambulizi mawili jana Alhamisi katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati ya Ukanda wa Gaza. Maafisa wa hospitali ya Al Aqsa wamesema miili inaendelea kupokelewa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW