1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lebanon yakamilisha awamu ya kuipokonya silaha Hezbollah

8 Januari 2026

Jeshi la Lebanon limesema limekamilisha awamu ya kwanza ya mpango wake wa kupokonya silaha kundi la Hezbollah kusini mwa nchi hiyo, hatua ambayo Israel imeitaja kuwa ya matumaini lakini "bado haitoshi”.

Lebanon
Licha ya makubaliano, Israel imeendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Lebanon, ikidai inalenga wapiganaji wa Hezbollah.Picha: Adri Salido/Getty Images

Hatua hiyo inajiri chini ya shinikizo kubwa kutoka Marekani na hofu ya kuongezeka kwa mashambulizi ya Israel. Jeshi la Lebanon limesema awamu ya kwanza imelenga eneo lililo kusini mwa Mto Litani, isipokuwa maeneo ambayo bado yanakaliwa na wanajeshi wa Israel karibu na mpaka.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, yuko Beirut kwa mazungumzo kuhusu kile anachokiita tishio la Israel katika eneo hilo. Huku Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, akiunga mkono hatua za jeshi, akisema lengo ni kuhakikisha serikali pekee ndiyo yenye mamlaka ya kubeba silaha na kufanya maamuzi ya vita na amani.

Hezbollah, inayoungwa mkono na Iran, ilidhoofika baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mapigano, yaliyohitimishwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi Novemba mwaka 2024.

Licha ya makubaliano hayo, Israel imeendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Lebanon, ikidai inalenga vituo na wapiganaji wa Hezbollah.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW