1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la Israel limewaua waandishi wa habari watatu

25 Oktoba 2024

Lebanon imesema shambuizi la anga la Israel, limewaua waandishi wa habari watatu leo ijumaa, kusini mwa nchi hiyo.

Shambulio la anga la Israeli laua waandishi wa habari watatu kusini mwa Lebanon, huko Hasbaya.
Shambulio la anga la Israeli laua waandishi wa habari watatu kusini mwa Lebanon, huko Hasbaya. Picha: Stringer/REUTERS

Wizara ya habari ya Lebanon imelitaja shambulizi hilo kuwa ni uhalifu wa kivita. Kituo cha Televisheni cha Lebanon kinachoegemea Iran cha Al Mayadeen kimeripoti kuwa mpiga picha na fundi mitambo wameuawa katika shambulizi lililolenga makazi ya waandishi katika eneo la Hasbaya kusini mwa nchi. Kituo kingine cha Al-Manar kinachoendeshwa na Hezbollah, kimesema mwandishi wake mmoja pia ameuawa. Waandishi wa habari kutoka mashirika mengine ya vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na Televisheni ya Lebanon ya Al-Jadeed, Idhaa ya Kiarabu ya Sky News na ile ya Kiingereza ya Al Jazeera, pia walikuwa wamepumzika karibu na eneo hilo wakati kulipotokea shambulizi usiku wa kuamkia leo.