1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lebanon yatoa wito kusitishwa vita vya Israel na Hezbollah

11 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati ameutolea mwito Umoja wa Mataifa leo Ijumaa, kupitisha azimio la kusitishwa vita kati ya Israel na Hezbollah.

Libanon Najib Mikati
Picha: Mohamed Azakir/REUTERS

Mikati amewaambia waandishi habari kwamba wizara ya mambo ya nje italiomba baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutowa azimio la kutaka usitishaji kamili wa vita na kwamba serikali yake inaendelea kuliunga mkono azimio nambari 1701 lililopitishwa mwaka 2006.

Kadhalika waziri mkuu Mikati ametowa mwito wa jeshi la nchi yake na kikosi cha kulinda amani kuwa vikosi pekee vyenye silaha vitakavyopelekwa Kusini mwa nchi hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW