Lecornu ajaribu kuepusha mkwamo wa kisiasa Ufaransa
7 Oktoba 2025
Juhudi za Lecornu zinalenga kuiondoa nchi hiyo kwenye mkwamo wa kisiasa.
Rais Emmanuel Macron alimkabidhi Lecornu, mwenye umri wa miaka 39, jukumu la kuunda serikali mwezi uliopita baada ya bunge kumng'oa mtangulizi wake kufuatia bajeti ya kubana matumizi iliyokosolewa vikali.
Lecornu alitangaza baraza jipya la mawaziri Jumapili jioni, lakini likakosolewa kwa kuwa na sura nyingi zilezile kutoka serikali iliyopita. Hali hiyo ilimfanya achukue uamuzi wa kujiuzulu mapema Jumatatu.
Katika hatua ya kushangaza, licha ya kukubali kujiuzulu kwake, Rais Macron amemwagiza Lecornu kutumia siku mbili zijazo kujaribu kuiokoa serikali yake.
Lecornu anatarajiwa kukutana na viongozi wa vyama leo katika ofisi ya waziri mkuu, kwa lengo la kutafuta suluhu ya kisiasa na kuondoa mkwamo uliopo.