1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lecornu asimamisha mpango wa pensheni Ufaransa

14 Oktoba 2025

Waziri Mkuu wa Ufaransa Sebastian Lecornu leo ameusimamisha mpango wa Rais Emmanuel Macron wa mwaka 2023 wa kuongeza muda wa kustaafu hadi miaka 64, mpaka baada ya mwaka 2027.

Waziri Mkuu wa Ufaransa Sebastien Lecornu
Waziri Mkuu wa Ufaransa Sebastien LecornuPicha: Stephane Mahe/REUTERS

Lecornu amechukua hatua hiyo kutokana na shinikizo alilowekewa na wabunge wa mrengo wa kushoto, waliokuwa wamemtaka achukue hatua hiyo ili aweze kusalimika kisiasa.

Waziri mkuu huyo anayekabiliwa na kibarua cha kunusurika kura mbili za maoni wiki hii, ametangaza hilo bungeni kama sehemu ya hatua ya mwisho ya kujaribu kuweka mazingira ya kupitisha bajeti ya mwaka 2026.

Ufaransa iko katika mgogoro mbaya zaidi wa kisiasa kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miongo kadhaa huku Lecornu akiwa waziri mkuu wa sita kuteuliwa na Rais Emmanuel Macron katika kipindi cha miaka miwili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW