1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leipzig na Stuttgart watinga nusu fainali DFB Pokal

6 Aprili 2023

Mabingwa watetezi wa kombe la shirikisho nchini Ujerumani DFB Pokal, RB Leipzig, wameyaweka hai matumaini yao ya kunyakua ubingwa kwa mara ya pili mfululizo, baada ya kuwalaza Borussia Dortmund 2-0

DFB-Pokal - RB Leipzig walipokutana na Borussia Dortmund
Wachezaji wa RB Leipzig wakishangiliaPicha: RONNY HARTMANN/AFP

Mabingwa watetezi wa kombe la shirikisho nchini Ujerumani DFB Pokal, RB Leipzig, wameyaweka hai matumaini yao ya kunyakua ubingwa kwa mara ya pili mfululizo, baada ya kuwalaza Borussia Dortmund 2-0 na kujikatia tiketi ya nusu fainali katika mechi iliyochezwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Redbull Arena huko Leipzig.

Wenyeji Leipzig waliingia uongozini katikati ya kipindi cha kwanza baada ya Mohamed Simakan kumuandalia pasi safi kabisa Timo Werner ambaye aliusindikiza wavuni mpira. Kunako kipindi cha pili na mwishoni mwa muda wa ziada, beki Willi Orban aliugonga msumari wa mwisho katika jeneza la Dortmund kwa kuwafungia Leipzig goli la pili na kuwapeleka katika hatua ya nne bora. Kwengineko mapema jana Enzo Millot alifunga goli la pekee mechi ilipokuwa inaelekea ukingoni na kuipelekea VfB Stuttgart kuizamisha Nuremberg 1-0 na kuibandua nje ya mashindano hayo katika nusu fainali nyengine iliyochezwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW