Leipzig wapunguza pointi baina yao na Bayern Munich
26 Aprili 2021Kiungo wa Leipzig Emil Forsberg alikuwa na haya ya kusema baada ya ushindi huo.
"Tulitaka kushinda bila shaka, Jumanne nilisema kwamba tunataka kutoa jawabu. Nahisi leo tumecheza vizuri, bila shaka tulipata usaidizi kidogo kutokana na kadi nyekundu waliyopewa lakini tumecheza vyema, tukashinda na hilo ndilo la muhimu. Kwa sasa tumepata kujiamini kidogo, ulikuwa ushindi muhimu sana kwetu," alisema Forsberg.
Mechi ya pili Jumapili ilishuhudia Borussia Mönchengladbach kuwafumania Arminia Bielefeld tano bila jawabu, ushindi ambao ulimfurahisha sana kocha wa Gladbach ambaye msimu ujao atakuwa anachukua mikoba ya kuiongoza Borussia Dortmund, Marco Rose.
"Nafikiri kwa sasa sistahili kupiga hesabu nyingi. Tuko pointi nne nyuma ya Leverkusen, bado kumesalia pointi tisa kuchezewa na hiyo inamaanisha ni sharti Leverkusen wateleze na sisi ni lazima tupate pointi katika mechi tatu zilizosalia tukianza na mechi tutakayocheza mjini Munich," alisema Rose.