Leo ni Marekani ama Japan
17 Julai 2011Matangazo
Marekani leo inajaribu bahati yake kuweza kunyakua kombe hilo kwa mara ya tatu, baada ya kufanikiwa kufanya hivyo mwaka 1991 na 1999.
Kwa upande wake, Japan ilipata ushindi wa kushangaza katika michuano hiyo, baada ya kuwatoa wenyeji na mabingwa watetezi wa kombe hilo, Ujerumani.
Jana Sweden iliweza kushika nafasi ya tatu ya michuano hiyo, baada ya kuifunga Ufaransa bao mbili kwa moja. Bao lake la ushindi lililofungwa na Marie Hammarström, lilipatikana dakika nane tu kabla ya mpira kumalizika.