1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leo ni siku ya kwanza ya 2024

1 Januari 2024

Mataifa katika maeneo yote ya ulimwengu yapo katika sherehe za kuukaribisha Mwaka Mpya, huku watu wengi wakitarajia nyakati bora licha ya mizozo katika maeneo ya Mashariki ya Kati, Ukraine na kwengineko barani Afrika.

Silvester & Neujahr 2023 - 2024 | Sydney, Australien
Picha: Roni Bintang/Getty Images

Eneo la Kanda ya Pasifiki ndiyo limekuwa ka kwanza kuingia katika mwaka wa 2024. Sehemu za Mashariki ya Mbali zimeukaribisha 2024 kwa maonyesho makubwa ya fataki, ikijumuisha Seoul na Tokyo. Huko Japan, kengele za hekalu zililia kote nchini wakati watu wengi walipokusanyika kwenye mahekalu makubwa na madogo ya ibada kwa lengo la kukaribisha mwaka mpya.Jiji kubwa zaidi la Australia, Sydney, ambalo limejitangaza kuwa "Mji mkuu wa Mwaka Mpya wa ulimwengu." Kisiwa cha Kiribati miongoni mwa maeneo ya mwanzo kuadhimisha mwaka 2024, ingawa hakukukuwa na matukio makubwa ya maadhimisho yaliyopangwa katika kisiwa kikuu cha Kiritimati.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW