1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen waendelea kuwaumisha kichwa Bayern

15 Januari 2024

Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga ilianza tena mechi zake za awamu ya pili ya msimu baada ya mapumziko ya majira ya baridi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kandanda Bundesliga | FC Augsburg - Bayer Leverkusen
Exequiel Palacios akisherehekea goli la dakika ya mwisho dhidi ya AugsburgPicha: Leonhard Simon/REUTERS

Vinara Bayer Leverkusen wameendelea kuiongoza Bundesliga wakiwa pointi nne mbele ya watani wao Bayern Munich, baada ya ushindi mgumu na mwembamba wa 1-0 dhidi ya Augsburg.

Ushindi kwa Leverkusen katika mechi hiyo ulikuwa muhimu ukizingatia kwamba Bayern Munich walikuwa wamevuna ushindi wa 3-0 walipocheza na Hoffenheim siku moja kabla.

Ikumbukwe lakini Bayern hawajacheza mechi moja ila hata wakaishinda mechi hiyo dhidi ya Union Berlin, watakuwa pointi moja nyuma ya Leverkusen ambao kwa sasa pointi walizo nazo ni 45 kwa 41 za Bayern.

Kwa sasa Bayern wameanza mazoezi ya siku nne huko nchini Ureno ambako hali ya hewa ni nzuri kidogo ikilinganishwa na jimboni Bavaria ambako baridi ni kali mno.

Mshambuliaji wa Bayern Munich Harry KanePicha: Matthias Schrader/AP Photo/picture alliance

Kocha Thomas Tuchel amesema kikosi chake kitakuwa huko Algarve Ureno hadi Alhamis watakaporudi kujiweka tayari kuwakaribisha Werder Bremen Jumapili huko Allianz Arena.

Chanzo: Reuters/AP/AFP