1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen waufungua msimu wa Bundesliga kwa ushindi

24 Agosti 2024

Mabingwa Bayer Leverkusen waliendeleza walikoachia na kuanza msimu mpya wa Bundesliga kwa ushindi wa dakika za mwisho wa mabao 3 - 2 ugenini dhidi ya Borussia Moenchengladbach jana usiku.

Ujerumani | Borussia Moenchengladbach vs. Bayer 04 Leverkusen | Bundesliga 0:2
Leverkusen wameendeleza walikoachia kwa kuanza msimu mpya wa Bundesliga na ushindi wa 3 - 2 dhidi ya GladbachPicha: Joerg Niebergall/Eibner-Pressefoto/picture alliance

Msimu uliopita, Leverkusen ilishangaza kwa namna ilivyofunga mabao kadhaa ya dakika za lala salama na muhimu katika safari yao ya kushinda taji lao la kwanza la ligi kuu na kuumaliza msimu bila kupoteza mechi hata moja.

Na inaonekana muujiza huo wa dakika za majeruhi umerudi kwa msimu wa 2024-25. Mabingwa hao watetezi walikuwa kifua mbele 2 - 0 kabla ya Gladbach kupambana na kurejesha mabao hayo lakini Leverkusen ikapewa penalti katika dakika ya 10 ya muda wa nyongeza.

Soma pia: Bayer Leverkusen yabeba Kombe la Super Cup la Ujerumani

Katika mechi za Jumamosi, Stuttgart ambao walimaliza wa pili msimu uliopita watacheza dhidi ya Freiburg, RB Leipzig watakuwa nyumbani dhidi ya Bochum na Borussia Dortmund watawakaribisha Eintracht Frankfurt dimbani Signal Iduna Park. Jumapili, Bayern Munich wataanza msimu wao dhidi ya Wolfsburg.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW