1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen yachapwa 7 -2 na PSG

22 Oktoba 2025

Jumatano mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich watawakaribisha Club Brudge ya Ubelgiji huku Real Madrid wakimenyana na kibibi cha Turin Juventus. Mechi hizi zitachezwa majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

UEFA Champions League I 2025  Robert Andrich
Nyota wa Bayer Leverkusen Robert Andrich akipewa kadi nyekundu wakati wa mchezo wao dhidi ya PDGPicha: Meuter/nordphoto GmbH/picture alliance

Ligi ya mabingwa barani Ulaya imeendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali usiku wa kuamkia leo. Hapa Ujerumani Bayer Leverkusen wakiwa nyumbani Bay Arena walichapwa 7-2 na mabingwa watetezi wa kombe hili Paris Saint German, vigogo wengine wa Ujerumani Borrusia Dortmund wao waliwacharaza Copenhagen ya Denmark 4-2.

Barcelona yaUhispania waliinyeshea mvua ya magoli 6-1 Olympiacos ya Ufaransa huku Wahipania wengine Atletico Madrid wakiangukia pua kwa kuchapwa 4-0 na Arsenal ya England.

Hii leo, mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich watawakaribisha Club Brudge ya Ubelgiji huku Real Madrid wakimenyana na kibibi cha Turin Juventus. Mechi hizi zitachezwa majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW