1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lewandowski apachika magoli 4

5 Oktoba 2020

Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski alipachika wavuni magoli manne na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa magoli manne kwa matatu walipokuwa wakikwaana na Hertha BSC Berlin.

Fußball Bundesliga I FC Bayern Muenchen - Hertha BSC Berlin
Picha: Andreas Gebert/Reuters

Berlin walikuwa wana matumaini kwamba watachukua angalau pointi moja kwenye mechi hiyo baada ya kusawazisha mnamo dakika ya 88 ila Lewandowski alikuwa na mawazo mengine. Katika muda wa ziada ilipogonga dakika ya tisini na nne mshambuliaji huyo raia wa Poland aliweka wavuni goli la ushindi.

Hansi Flick ni kocha wa Bayern Munich.

"Leo tulikuwa tunataka pointi tatu zisalie hapa Munich na ukiangalia kisaikolojia timu yetu leo ilikuwa vizuri kwa sababu tulifungwa na kisha tukarudisha magoli na hata kuibuka na ushindi, kwangu mimi hilo ni jambo zuri sana," alisema Flick.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW