1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lewandowski ashinda tuzo ya FIFA ya mchezaji bora

18 Desemba 2020

Robert Lewandowski ameshinda tuzo kubwa kabisa ya taaluma yake, na kudhihirisha kuwa mshambuliaji ambaye sio Messi au Ronaldo anaweza kupigiwa kura ya kuwa mchezaji bora wa kandanda duniani.

The Best FIFA Football Awards | Robert Lewandowski FC Bayern München Weltfußballer
Picha: VALERIANO DI DOMENICO/POOL/AFP

Nahodha huyo wa Poland ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA Mwanaume katika mwaka wa 2020 baada ya mabao yake 55 ya msimu kuisaidia Bayern Munich kunyakua mataji ya kimataifa na ya nyumbani.

Lewandowski alipata kura 52 dhidi ya 38 alizopata Lionel Messi wakati Cristiano Ronaldo akipata 35. Hafla ya tuzo hiyo ilifanyika Zurich kwa njia ya video lakini Rais wa FIFA Gianni Infantino alikwenda hadi Munich kumkabidhi binafsi Lewandowski tuzo yake. Lucy Bronze wa Uingereza alishinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.

Alishinda Ligi ya Mabingwa akiwa na Olympique Lyonnais kabla ya kuhamia Manchester City. Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alimpiku Mjerumani mwenzake Hansi Flick wa Bayern Munich na Marcelo Bielsa wa Leeds katika tuzo ya kocha bora. Manuel Neuer alishinda tuzo ya kipa bora.

afp, dpa,reuters, dpa

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW