1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lewis Hamilton abaguliwa kirangi

19 Julai 2021

Lewis Hamilton alishambuliwa kwa matusi ya kibaguzi kwenye mitandao ya kijamii mara tu baada ya kushinda mashindano ya mbio za magari ya British Grand Prix hapo Jumapili.

British Grand Prix I Formel 1 I Silverstone
Picha: Peter Cziborra/REUTERS

Bingwa huyo mara saba aliweka rekodi baada ya kushinda kwa mara ya nane jana katika uwanja wa Silverstone. Aliibuka kidedea licha ya kuwa aliadhibiwa kwa kupunguziwa pointi kumi baada ya kugongana na hasimu wake Max Verstappen ambaye aliishia kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

"Ninawashukuru sana mashabiki. Ninaomba kila mmoja asalie kuwa mwenye afya na murudi nyumbani salama. Hii ni ndoto leo kuweza kupata ushindi huu mbele yenu nyote ila singeweza bila ya ushirikiano wa Valtteri na juhudi kubwa za timu nzima," alisema Hamilton.

Lewis Hamilton baada ya ushindi wakePicha: Andrew Couldridge/REUTERS

Katika taarifa ya pamoja, timu ya Mercedes yake Hamilton, Formula One na shirikisho linalosimamia mchezo huo wa magari ya langa langa FIA wamelaani matusi hayo dhidi ya Hamilton na wametaka waliohusika waadhibiwe.