1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Liberia: Mradi wa kuwasaidia vijana

17 Novemba 2015

Mradi wa 'Kick for Your Future' unaoendeshwa na taasisi ya YOCADS inayosaidia vijana wanaoishi katika mazingira ya watu wenye kipato cha chini kuweza kujikwamua kiuchumi

Screenshot Kick for the future Fostering young talent in Liberia Barbara Ketter
Picha: DW/D. Hirschfeld

Liberia: Mradi wa kuwasaidia vijana

03:12

This browser does not support the video element.

Emmanuel Effun anajua jinsi jenereta inavyofanya kazi na jinsi ya kuiunganisha. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akifanya kazi ya umakenika kama mwanafunzi katika kipindi cha miaka sita iliyopita. Ana msisimko kwa sababu mtu alimfundisha kazi Babra Ketter amefika katika karakana yake iliyoko nje kidogo ya mji wa Monrovia kuona jinsi Emanuel anavyo endelea. Babra anaendesha mradi unaojulikana kama Kick for Your Future unaoendeshwa na taasisi ya YOCADS ambayo inasaidia vijana nchini Liberia wanaoishi katika mazingira ya watu wenye kipato cha chini kuweza kujikwamua kiuchumi.