1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLiberia

Liberia yafanya uchaguzi wa rais na bunge

10 Oktoba 2023

Waliberali wanapiga kura leo Jumanne kuamua kama wampe muhula wa pili Rais George Weah.

Rais George Weah awania muhula wa pili madarakani Liberia.
Rais George Weah awania muhula wa pili madarakani Liberia.Picha: Peter Dejong/AP/picture alliance

Amani ndilo suala muhimu miongoni mwa wapiga kura mnamo wakati uchaguzi ukiendelea, katika nchi hiyo ambayo bado ina makovu ya vita mfululizo vya wenyewe kwa wenyewe.

Alipochaguliwa mwaka 2017 Rais Weah aliahidi kutengeneza nafasi za ajira na kuwekeza katika elimu, lakini wakosoaji wanasema ameshindwa kutimiza ahadi zake.

Weah ana nafasi kubwa ya kushind uchaguzi huo dhidi ya wagombea 19 wanaowania urais lakini huenda akakabiliwa na uchaguzi wa duru ya pili mapema mwezi Novemba ikiwa hakuna mgombea atakayepata wingi wa kura unaohitajika katika duru ya kwanza.

Mamia ya watu walijitokeza mapema Jumanne kupiga kura katika mji mkuu Monrovia.

Vyama vikuu vya upinzani vimeahidi kwamba uchaguzi wa rais na bunge utafanyika kwa amani. Uchaguzi huo ni wa kwanza kufanyika tangu Umoja wa Mataifa ulipokamilisha tume yake ya amani Liberia mnamo 2018.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW